Pages

Thursday, March 28, 2013

DIDA WA G AMPA MAKAVU LIVE SINTAH.

Sintah ambaye ni muigizaji na mtangazaji anaonekana kuwa na bifu na watu wengi wakidai anawafatafata huku Sintah mwenyewe akijitapa kuwa yeye ni mtambo wa kurekebisha tabia kupitia blog yake. Safari hii kunaonekana kuwa na bifu kati ya Sintah na mtangazaji maarufu wa muziki wa taarabu ambaye pia ni muimbaji wa muziki huo na pia actress Dida wa G, Dida amemjibu hivi Sintah.....

"WADAU KWELI MIMI NI MTU MZIMA WALA SI KIPANDE NA SIJAFIKIA UTU UZIMA UOOOO SABABU SICHAMBII PANGA WALA SIPIGI DANADANA KWA MAKALIO,ILA NAPENDA NIWATOE HOFU NYIE MNAOJIFANYA MNANIJUA SANA KULIKO MAMA YANGU MZAZI NI HIVI NAMTAJA LIVE SABABU ANAJUA SIMUHOFII WALA SIMUOGOPI NA SINA SHARI NAE ILA AKIITAKA KWANGU ATAINUNUA KWA BEI RAHISI BILA YA VAT,SINTA NAKUTAJA NA NAJUA HUWEZI CHAMBANA NA MIMI HATA ROBO MAANA NITAKUPA UMAARUFU WA MUDA MCHACHE MAANA HATA WA KUTATIZA KATIKATI YA MSAFARA WA RAISI UTACHUKUA MUDA,NYIE MNAOSEMA NAMUOGOPA SINTA ANALIJUA ILO KUWA SIMUOGOPI HATA KIDOGO NA NIKITAKA KUCHAMBANA NAE SI HUMU NAMTAFUTA KWA GHARAMA ZANGU TUCHAMBANE FACE TO FACE KWA HIYO SINTA FANYA YAKO ANDIKA YAKO UMO KWENYE BLOG YAKO KWELI MIMI MTOTO WA KISWAHILI SINA UZUNGU HATA ROBO ILA UKINICHOKONOA UTAJUA KAMA MIMI MZUNGU AU MZARAMU NYIE WAZUNGU ENDELEENI NA UZUNGU WENU KWANGU NDIO KWANZA MKOKO UMEALIKA MAUA,KUMBUKENI MATUSI YENU HAYANITOI KOPE NDIO KWANZA ZIMENISIMAMA KAMA KIBANDA CHA SIMU."
Dida wa G

No comments:

Post a Comment