Pages

Thursday, March 28, 2013

STEPS WAANDAA TAMASHA LA FILAMU SWAHILIWOOD, KUTOA TUZO KWA WASANII NA FILAMU BORA NA PIA KUMUENZI KANUMBA.

Kampuni ya Steps Entertainment ambayo ni moja kati ya kampuni za usambazaji wa films za Swahiliwood ipo katika maandalizi ya kufanya tamasha la filamu mwezi ujao katika viwanja vya leaders jijini Dar es salaam. Mmoja wa wahusika kutoka Steps akizungumza na mtandao wa Bongomovies alisema kuwa tamasha hilo lina lengo la kukuza na kuendeleza tasnia ya filamu nchini, pia katika tamasha hilo wasanii na filamu zilifanya vizuri kwa mwaka 2012 zitapewa tuzo. Vile vile marehemu Steven Kanumba ataenziwa kupitia tamasha hilo kwa mchango wake mkubwa katika tasnia hiyo. Tamasha hilo litahusisha wadau wote wa films na wananchi wanaombwa wajitokeze kwa wingi siku hiyo. Tarehe ya tamasha hilo itatangawa hivi karibuni katika media.

                                                              The late Steven Kanumba

No comments:

Post a Comment