Sunday, January 20, 2013
EXCLUSIVE INTERVIEW WITH ACTRESS SALMA JABU(NISHA)
muigizaji wa Swahiliwood Salma Jabu famously known as Nisha ni actress asiyekauka kwenye media hasa magazeti ya udaku.Nisha aliyejaaliwa macho yenye mvuto wa gharama kubwa ameshaigiza filamu kibao na mastaa mbalimbali ikiwemo mpya ya Pusi na Paku. Exclusively swahiliworldplanet imekuletea mahojiano mafupi na actress huyu mwenye makeke mengi.
SWP:Je ni kweli wasanii wa kike hasa underground huwa wanaombwa rushwa ya ngono ili wapate nafasi ya kuigiza katika filamu?
NISHA:Sina hakika na siwezi sema yes or no because sijakutana nalo wakati naanza kuigiza filamu.
SWP: Ni muongozaji gani wa filamu Tanzania unakubali sana kazi zake? na kwanini hakuna ma-director wengi wa kike Tanzania tofauti na madirector wa kiume?
NISHA:Namkubali sana Mtitu wa Game First Quality kwa upande wa wanaume kwa upande wa kike Lamata ndio the best director kwangu.Hakuna ma-director wengi wanawake because ku-direct ni kipaji. Pia ni lazima uwe na uhakika na unachotaka kukiongoza na siyo kukurupuka tu.
SWP:Ni kweli mmeachana na aliyekuwa mpenzi wako singer Ney wa Mitego na sababu ni nini?
NISHA:Tumeachana tu hakuna sababu nafikiri.
SWP:Uhusika gani unaota kuucheza(dream role) katika filamu ambao bado hujaucheza mpaka sasa?
NISHA:Tayari nimecheza zote hakuna uliobaki
swp:ni sehemu gani ya mwili wako inadatisha sana mashabiki wako hasa wa kiume?
NISHA:Mashabiki wangu watakuwa wanadata na kazi zangu na siyo sehemu ya mwili wangu
SWP:Muigizaji gani wa kike Tanzania unakubali sana kazi zake?ni filamu gani inayokuja ambayo unafikiri umecheza vizuri sana mashabiki wako wakae mkao wa kula?
NISHA:Nawakubali wote wapo juu.filamu ni PUSI NA PAKU, mashabiki wenyewe wata-comment watakapoiangalia kuliko mimi kuanza kujisifia.
SWP::Washukuru watu 3 tu kwa kukusaidia kufika ulipo sasa kama muigizaji maarufu.
NISHA:I would like to thank my God,pili mama yangu,tatu walimu na ma-directors wangu wote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment