Tuesday, December 3, 2013

PHOTOS: WASANII WA FILAMU PATRICK BASHIZI NA MAGIE SELUWA WAFUNGA NDOA NCHINI DENMARK.

Patrick Bashizi na Maggie Seluwa ambao ni wasanii wa filamu za Kiswahili na wanamuziki wakiwa na makazi yao Norway wamefunga ndoa nchini Denmark juzi tarehe 30 mwezi November. Harusi hiyo ambayo ilikuwa na shamra shamra nyingi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki ilihitimisha ahadi ya wawili hao ya kuishi pamoja kama mke na mume kwa kuuaga ulimwengu wa mabachela. Angalia picha jinsi walivyomeremeta............

Hongereni sana kwa kuwa mabalozi wazuri wa Afrika kwa kuvaa vionjo vya kiafrika katika tukio hili muhimu licha ya kuwa Ulaya
Kila la kheri katika maisha mapya ya ndoa lakini mkumbuke bado tunawahitaji katika sanaa ya filamu na muziki kama kawaida.


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment