Thursday, April 7, 2016

Patrick Bashiz Adaiwa Kufundishwa Mambo Ya Freemanson Na Walter Anga Wa Nollywood Huko Norway !

Kwa mujibu wa chanzo ambacho hakikutaka jina lake lianikwe, msanii Patrick Bashiz ambaye hufanyia shughuli zake nchini Norway hivi majuzi alitembelewa na mmoja wa watu wake wa karibu aitwaye Walter Anga ambaye ni msanii wa Nollywood nchini Nigeria, Lakini habari zinadai kuwa Walter alienda Norway mahsusi kwa ajili ya kumfundisha Patrick mambo ya Freemanson ili afanikiwe katika kazi zake. Chanzo kinazidi kusema kuwa hata walipokuwa pamoja wawili hao ishara zao ni za ki-freemanson tupu.

Patrick Bashiz ambaye ni muigizaji, producer na director wa kampuni ya Nollywood Eourpe & JDP Productions alipotafutwa na kuulizwa juu ya madai hayo alisema....
Bashiz akiwa na mkewe pamoja na Walter Anga katika event ya Movie Premiere iliyofanyika hivi juzi hiko Norway.


"sijaaelewa kwanini watu wa dunia ni waongo sana, mimi sijawahi kuingia Freemanson, ni kazi tu nafanya na kipaji ambacho kanipa Mungu, ndani ya kazi zangu namuweka Mungu mbele, kuhusu brother Anga yeye ni superstar yaani nyota anayeng'ara kila mtu anamjua, leo nyota yangu imeng'ara wanadhani ni ushirikina ila Mungu ni mkubwa, hata pozi zangu katika hiyo picha sikufikiria hata kidogo nashangaa ulivyoniuliza, ukipata nafasi ya kuzungumza na brother Anga muulize haya na atakujibu kama nilivyokujibu, Mungu ni mkubwa hakuna zaidi yake."

Katika hatua nyingini Bashizi amesema kuwa kwasasa wapo katika mawasiliano na waigizaji wawili wa Nigeria ili mambo yakienda sawa wafanye kazi pamoja. Hivi majuzi pia Bashiz walizindua movie yao mpya picha ni hizo hapo chini wakiwa na dress code ya white...
Patrick Bashiz akiwa kwenye red carpet na mtangazaji maarufu wa Swahili Talk Radio ya Denmark Rehema Nkalami.


No comments:

Post a Comment