Sunday, December 6, 2015

Timoth Conrad, Omary Clayton Na Filamu Ya Dogo Masai Wang'ara Califonia Viewers Choice Awards 2015.

Ninaitwa Timoth Conrad Kachumia Director, Producer na Writer wa filamu Tanzania, Ninayofuraha kuwajulisha watanzania kuwa nimefanikiwa kushinda California Viewers Choice Awards 2015, tuzo 2 ikiwa ni Best Feature Film pamoja na Best Director kupitia filamu ya DOGO MASAI, vile vile kutoka katika filamu hiyo hiyo Omary Clayton ambaye ni muigizaji mkuu amefanikiwa kushinda tuzo ya Best Actor.
FIlamu ya Dogo Masai ni filamu ambayo inamzungumzia kijana mdogo ambaye anapitia wakati mgumu baada ya kudhulumiwa mali zake na Mjomba wake, hivyo anajikuta akiuvaa uhusika wa kimasai kutokana na kutupwa porini na kuokotwa na wamasai, Dogo Masai ni jina alilolitumia wakati wote kwenye filamu.

Upatikanaji wa washindi ulifanyika kupitia kura za mitandaoni na watu mbali mbali walionyesha kusapoti sana kwenye hatua ya kupiga kura na hatimaye kutuwezesha kushinda tuzo hizo ambazo ni za heshima kwa sababu zinatokana na majibu ya watazamaji wa filamu, filamu zote za washiriki zilionyeshwa online kwenye mtandao wawww.cvcawards.com na kupigiwa kura. Hivyo kura zimekusanywa kutoka kwa watazamaji wa kwenye mtandao.

List nzima ya washindi ipo hapa

Sambamba na tuzo hizo nina habari njema sana kwa watanzania nitakazozitoa kuanzia tarehe 20 december, kwani bado nipo hapa Los Angeles, California, USA. Ikumbukwe pia nilishinda tuzo za Silicon Valley African Film Festival kupitia filamu ya Single Zero mwaka huu huu.

List nzima ya washindi kwenye Silicon Valley African Film Fesitival 


No comments:

Post a Comment