Pages

Saturday, December 6, 2014

Sikumpiga Mke Wangu Bali Kaniundia Zengwe La Segerea Ili Aniibie Mali: Mtunisy

Mtunisy
Mtunisy Nice Mohamed ambaye ni star mkubwa wa filamu Tanzania amefunguka exclusively kuhusu issue yake ya kutupwa Segerea wiki hii mwanzoni ikidaiwa alimdunda vilivyo mkewe kiasi cha kunyimwa dhamana kwasababu mke huyoa alikuwa bado katika hali mbaya.


Hata hivyo Swahiliworldplanet imefanya juu chini kumpata star huyo ambaye anatarajiwa kutikisa soko na filamu yake mpya ya Tugawane Maumivu. Mtunisy alipododoswa alisema kuwa aligombana kawaida tu na mke wake huyo kama wanandoa wengine ila mke wake huyo aliamua kumuundia zengwe kuwa alimpiga wakati hakumpiga wala nini na kisha mke huyo kumfungia dhamana, Mtunisy alisema kuwa mke wake huyo alikuwa na tamaa za kuchukua mali zake.

"Ukweli ni kuwa niligombana na mke wangu kawaida tu na sikumpiga, aliamua tu kunifungulia mashitaka ya kumpiga na kunifungia dhamana nikapelekwa Segerea, wakati nipo huko Segerea wao wakenda kuniibia vitu vyote ofisini, shida yake ilikuwa mali ndio maana akaniweka ndani ili apate njia ya kuniibia" alisema Mtunisy anayedaiwa kuwa mmoja wa mastaa wa kiume Tanzania wenye mvuto mkubwa kwa wanawake


No comments:

Post a Comment