Sunday, November 9, 2014

T.I.D Kuja Na Girlfriend 2, Sabby Angel Kucheza Character Ya Monalisa.

Sabby Angel na T.I.D
Sabby Angel na T.I.D Filamu maarufu ya Girlfriend iliyotengenezwa kati ya mwaka 2002/2003 na kuleta mapindui ya filamu za kibiashara nchini Tanzania na kuchochea kukua kwa tasnia ya filamu nchini inatarajiwa kutengenezwa sehemu ya 2.

 Girlfriend original ilikuwa inazungumzia maisha na wasanii wa muziki wa kizazi kipya huku waigizaji wakuu wakiwa ni T.I.D, Monalisa Yvonne Cherry, Ay, Nina Beatrice Morris, Sauda Kilumanga, Jay Moe, Bakari Makuka na Ndende. Habari mpya ni kuwa T.I.D ambaye wimbo wake wenye jina hilo ndio ulizaa wazo la filamu hiyo iliyoongozwa na marehemu George Tyson anakuja na sehemu ya 2 ya Girlfriend.

 Akizungumza na Millardy Ayo mwanamuziki huyo maarufu amesema yupo katika mchakato wa movie hiyo huku nafasi ya mhusika mkuu mwanamke ambayo ilichezwa na Monalisa sasa itachezwa na Sabby Angel ambaye licha ya kuwa muigizaji wa filamu za Hard Price, Siri Ya Giningi, Moto Wa Radi na Sio Riziki lakini pia ni mwanamuziki wa kizazi kipya pia akitarajiwa kuonekana katika video mpya ya T.I.D iitwayo chumvini. 

No comments:

Post a Comment