Wednesday, November 5, 2014

Simu Ya Timoth Conrad Yaibiwa Na Kutumika Kutapeli Watu.

Ikiwa bado Timoth Conrad ‘Tico’ hajarudi kutoka nchini Marekani alikoenda kwa ajili ya Tuzo za SVAFF. Leo zimesambazwa sms kutoka kwenye namba ya simu yake ya mkononi aliyokua akiitumia alipokua nchini Tanzania.

image
Ujumbe unaotumwa
Ujumbe huu unatumwa kutoka kwenye namba ya Tico inayoishia na 6661 pamoja na 1498 laini zote mbili zilikua kwenye simu moja.
“Imekua kama bahati nilikua nachati na Faridi Uwezo kwa kutumia Facebook akaniuliza kama nimerudi au laa, nilipomjibu kua sijarudi akashangaa na kunieleza kua amepokea ujumbe wakumuomba pesa kutoka kwenye namba yangu ya Bongo” alisema Tico akiwa Califonia Marekani.
image
Timoth Conrad 'Tico'
Hata hivyo aliendelea kwa kusema kua baada ya hapo akafanya mawasiliano kwa mchumba wake ambaye yupo Bongo na ndiye aliyekua na simu hiyo, ndipo akaambiwa kua ni kweli simu yake iliibiwa na mtu asiyejulikana. Na ikipigwa bado inaita inamaana ipo hewani.
Kama kuna mtu wa karibu na Tico na ametumiwa ujumbe huu tafadhali toa ushirikiano ili kumkamata mwizi kwa kupiga namba 0714623966.
image
Timoth Conrad akiwa Nchini Marekani

No comments:

Post a Comment