Saturday, November 8, 2014

Photos: Vj Penyy Na Wema Sepetu Wamaliza Beef Lao Lililosababishwa Na Penzi La Diamond Platnumz.

Vj Penny na Wema Sepetu baada ya kupatanishwa
Yaliyopita si ndwele tugange yajayo !.....well, waliokuwa mahasimu wakubwa Wema Sepetu na Vj Penny wameondoa beef lao lililotokana na Penny kumuingilia Wema katika penzi la Diamond Platnumz miezi kibao iliyopita kabla ya mwishoni mwa mwaka jana Wema kufanikiwa tena kumrudisha Diamond katika himaya yake.

Wema na Penny walipatanishwa jana na rafiki yao aitwaye Junaithar ambapo ilikuwa birthday yake huku akiwaalika marafiki hao wa zamani na kisha kuwapatanisha na kuweka picha Instagram wakiwa wote kama zinavyoonekana.

"Wema na Penny leo wamemaliza tofauti zao, nilimjua Wema kupitia Penny, nawapenda sana wadogo zangu@Wema Sepetu_ Aunty Ezekiel @Vj Penyy04 @nsepetu" aliandika Junaithar kupitia Instagram

Kwasasa Vj Penyy amechumbiwa na mwanaume ambaye watu bado kumjua baada ya kumwagana na Diamond Platnumz mwishoni mwa mwaka jana

Vj Penny, Junaithar na Wema Sepetu baada ya kupatanishwa

No comments:

Post a Comment