Pages

Saturday, November 22, 2014

Ndoa Ya Batuli Yapamba Moto, Tarehe Rasmi Kutangazwa Siku Chache Zijazo.

Batuli
Star wa filamu Tanzania Batuli Yobnesh Yusuph anatarajia kufunga ndoa siku si nyingi baada ya kupata mwandani wa maisha yake.
Akizungumza na Globalpublishers Batuli ambaye anatarajiwa kuonekana katika filamu mpya akiwa na Ray Vicent Kigosi amesema kuwa wasanii wanachangamoto kubwa katika suala la ndoa kutokana na baadhi yao kuwa na skendo ila yeye anamshukuru Mungu kulivuka hilona sasa anataka kuingia katika maisha ya ndoa

"Ndoa siyo kitu cha mchezo tena kwa sisi wasanii mambo ni mengi. Kazi yetu tunakutana katika mazingira mbalimbali hatarishi na wadau tofauti, vikwazo ni vingi na mtu akivuka salama basi ni jambo la kumshukuru Mungu"

Alipoulizwa lini hasa ndoa yake itafungwa actress huyo aliyejaaliwa mvuto licha ya kuwa na watoto wawili alisema "Wewe usijali, utakuwa wa kwanza kualikwa. Tena Desemba 5 nitakuita umuone mume wangu mtarajiwa, nitakutambulisha kwa majina na kila kitu, baada ya hapo nitakupa tarehe kamili ya ndoa yangu maana kila kitu kimeshakaa kwenye mstari, soon tu nitakuwa mke wa mtu"

No comments:

Post a Comment