Pages

Saturday, November 22, 2014

Mimi Ni Mzuri Kuliko Demu Yeyote Bongo Msionikubali Shauri Yenu: Wema Sepetu

Wema
kwa wale ambao bado hawamkubali Wema Sepetu kuwa ni mzuri wa haja sasa star huyo anadaiwa kuwashukia.

 Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilicho karibu na Wema Sepetu kimesema kuwa Wema anaamini yeye ni mzuri sana na hakuna demu yeyote wa kumbabaisha kunako anga za uzuri Bongo!. Kikichonga na Swahiliworldplanet jana jioni chanzo hicho kilisema kuwa kuna baadhi ya watu hawaishi kumkosoa Wema hata baada ya kuachana na mkorogo ambao waliushupalia kuwa ndio ulikuwa ukimtoa na kuwaka mjini.

 "Madam(Wema Sepetu) anaamini yeye ni mzuri sana kuliko demu yeyote Bongo ndio sababu alitwaa crown Miss Tanzania, unajua kuna people hawaishi kumkosoa licha ya kuacha mkorogo...ooh Wema si mzuri...ooh Wema shape yake sio original..oh hivi na vile, jamani Wema anajikubali hakuna level yake kwa uzuri, she is hot sababu kila mwanaume anambabaikia, anasema wasiomkubali shauri yao" kilisema chanzo ambacho mara kadhaa huonekana na Wema kwenye events mbalimbali. 

No comments:

Post a Comment