Monday, November 17, 2014

Mmasai Amposa Wema Sepetu, Diamond Alikuwa Kikwazo Kwake.

Wema na Mmmasai aliyemposa 
Mmasai anayejulikana kwa jina la Ayoub Nyembo ameenda nyumbani kwa kina Wema Sepetu kwa lengo la kumposa star huyo mkubwa nchini.
Jamaa huyo alikuwa akimpenda Wema kwa muda mrefu na aliposikia hivi juzi kuwa wameachana na Diamond moyo wake ulijawa na furaha kuwa nafasi yake ya kumposa Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 ndo hii. Kwa mujibu wa Globalpublishers Mmasai huyo aliongozana na mshenga wake mpaka nyumbani kwa mama Wema yaani Sinza- Mori. Mama Wema alifurahi Mmasai huyo na kutaka kumuoa Wema kwa kumuuliza "Kwa hiyo Wema wangu anatakiwa aolewe Kigoma akale migebuka eeh?"

Mshenga wa mmasai alijibu "Ndiyo mama, Masai anaishi Kigoma ila ana nyumba zake Dar, huwa anakuja mara kwa mara kwenye biashara zake na pia ana mji Singida katika Kijiji cha Ikungi na ni mfugaji mzuri, ng’ombe anao wa kutosha.”
Mmasai akiwa na Mshenga wake karibu na kwa kina Wema Sepetu.

Mama Wema alifurahi kusikia Mmasai huyo ana kijiji tena anachotokea mama Wema hivyo kumtaka jamaa huyo kufuata taratibu za kitanzania katika kumposa Wema kwa kuzungumza na Wema mwenyewe kwanza na akikubali ndiyo arudi kwake yeye mama Wema. Barua ya posa ya Mmasai huyo iliandikwa kwa kiarabu na posa yake ilikuwa shilingi elfu hamsini.
"Hili ni jambo la kheri jamani, nimekuelewa lakini uchukue barua hii sambamba na posa urudi kwanza ukamwambie huyo mkwe mtarajiwa azungumze na Wema wakikubaliana, Wema yeye ndiye aniambie siku ya ninyi kuja kutoa posa ili na mimi nijiandae," alisema mama Wema

                                                Barau ya posa ya Mmasai huyo

No comments:

Post a Comment