Friday, November 7, 2014

Chausiku Ya Shamsa Ford Yavunja Rekodi Ya Kanumba Sokoni, Awagaragaza Ray Na JB.

Shamsa Ford amevunja ile kasumba kuwa waigizaji wa kiume ndiyo wenye nguvu sokoni baada ya filamu yake ya Chausiku kupendwa na kuuza sana mwaka huu 2014 kiasi cha kufikia na kuivunja rekodi ya hayati Steven Kanumba kupitia filamu yake ya Love And Power.
Filamu hiyo ambayo imeongozwa na JB imetokea kupendwa na watu kutokana na kuubeba uhalisia wa kitanzania hasa maisha ya watu wa mjini maeneo ya uswahilini.

Kwa mujibu wa Bongo5 afisa masoko wa kampuni ya Steps Entertainment, Ignatius Kambarage amesema kuwa filamu hiyo imeuza sana tangu itoke mwezi ulopita na bado inaendelea kuuza sana......

"Filamu ya Chausiku ndio imeweza kufika ile spidi ya filamu ya mwisho ya Kanumba "Love And Power", tumeuza sana, kama Steps tungekuwa tunatoa tuzo basi hii filamu ingepata tuzo. unajua watanzania sasa hivi wamebadilika wanatambua filamu hii nzuri hii mbaya, kwahiyo sasa hivi hawaangalii jina tena ni story pamoja na wahusika walivyovyaa uhusika wao"

Filamu hiyo ukiachilia mbali Shamsa Ford muigizaji mkuu wa kiume ni Rammy Galis huku wakisaidiwa na Cathy Rupia, Mayasa Mrisho na Annasiri Msangi. Chausiku ndiyo inaonekana kuwa filamu iliyouza sana mwaka huu huku Shamsa Ford akiwapiga vikumbo Ray na JB ambao ndiyo wanadaiwa kulishika soko kwa filamu zao kuuza sana

Swali ni je kama filamu hiyo imeuza sana na bado inaendelea kuuza kwanini mauzo yake yasiwekwe wazi maana kwa wenzetu wa Hollywood, Bollywood na hata Nigeria imeanza huweka wazi mauzo ya filamu maana industry ndivyo inavyotaka na hapa kwetu mambo kufanyika kienyeji na kwa kificho sana kuhusu mauzo ya filamu! .

 Suala hili bado linaleta mkanganyiko hasa kwasababu kuna kampuni nyingine pia filamu zao huuza sana na bado mauzo hayawekwi wazi mfano ni filamu ya Kigodoro na Mwali Wa Kizaramo ambazo pia mwaka huu zimetokea kupendwa sana na kuuza sana pia. Tunaamini kuwa kama mauzo ya filamu hayawekwi wazi na filamu nyingine huweza kuuza sana kupita matarajio wasanii ndiyo watazidi kuendelea kulalamika kunyonywa kwani wasanii bado wana kilio hicho mpaka sasa kuwa filamu nyingi hulipwa pesa inayofanana hata kama filamu flani ilizidi mauzo sokoni

No comments:

Post a Comment