Tuesday, October 28, 2014

TAFF Waja Na Tuzo Kubwa Za Filamu Nchini "Tanzania Film Awards", Kufanyika February 2015.

Kampuni ya Binary and Pixels Ltd. kwa kushirikiana na Shirikisho la Filamu Tanzania-TAFF wanaanzisha Tuzo kubwa za Filamu nchini (Tanzania Film Awards-TAFA) zitakazofanyika tarehe 28 Februari 2015.

Mchakato wa kuchukua fomu za kuwania Tuzo hizi za TAFA utaanza rasmi tarehe 1 hadi 30 Novemba 2014, na uzinduzi rasmi wa kampeni kwa Tuzo hizi utafanyika tarehe 21 Novemba 2014.

Ukiwa mdau (mtengenezaji filamu, muongozaji, muigizaji, mwandishi wa filamu, mpigapicha, mhariri wa filamu nk) unaombwa kushiriki kwenye Tuzo hizi kubwa ambazo hazijawahi kufanyika nchini, fomu za ushiriki zitapatikana kwenye ofisi za TAFF, Kinondoni au kwenye wavuti ya Shirikisho: http://www.taff.or.tz/

No comments:

Post a Comment