Monday, October 6, 2014

Nimejitoa Pia Club Ya Bongo Movie Unity Haina Faida Na Maana Yoyote: Sandra

Sandra
"Jamani siku zote mtu nafanya kazi kwa kutegemea faida, kwangu mimi imekuwa hasara, na mimi na family na watoto na mume, mume wangu ameniruhusu kujiunga na club ya Bongo movIe kwa kujua nitapata faida kupitia clabu hii,
nimekaa miaka mitatu mpaka Leo sioni nililolipata zaidi ya unafiki watu kwenye mambo ya pesa wanachaguana wenyewe kwa wenyewe sioni haja ya kuendelea kupoteza muda wangu bila faida kuanzia leo nimejitoa rasmi sio mwana chama tena wa Bongo movie nitakuwa msanii wa kawaida mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" ameandika Sandra Salama Salmini kupitia Instagram

Kundi la Bongo movie Unity ni sehemu ya kikundi kidogo tu katika tasnia ya filamu nchini wasanii wa kundi la Bongo movie unity wengi ni wale wenye majina huku wasanii wengi wakiwemo wale wachanga kuweka nguvu na matumaini yao katika Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) ambalo ndio kubwa na chombo mama cha tasnia ya filamu nchini, mikakati yake ni kupigania maslahi ya wasanii wote na tasnia ya filamu nchini kwa ujumla, TAFF inaundwa na vyama mbalimbali vya wasanii wa filamu nchini lakini kundi la Bongo movie unity inadaiwa sio mwanachama sababu zikidaiwa ni kujiona ni maarufu na kila kitu huku wakiishia. Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ni Simon Mwakifwamba huku aliyekuwa mwenyekiti wa kundi au club ya Bongo Movie Unity Steve Nyerere akijiuzulu hivi karibuni kwa madai ya kula pesa za kundi hilo kinyume na taratibu

No comments:

Post a Comment