Wednesday, October 22, 2014

Toyota-Coasta 25 Zajazwa Mashabiki Wa Ali Kiba kwenda Kumzomea Diamond Kwenye Fiesta !

Ali Kiba na Diamond Platnumz
Mtifuano! Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 limepita lakini nyuma yake limeacha vita nzito iliyowahusisha mafahari wawili, Diamond Platnumz na Ali Kiba 

Msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba akipafomu.
TIFU LILIVYOKUWA
Kwa mujibu wa
Globalpublishers Kwenye shoo hiyo iliyofanyika wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar, mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Ali Kiba (Team Kiba), walipiga kelele za ‘buuu’ pale alipopanda Diamond kutumbuiza ili kumharibia.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
CHANZO CHANENA
Chanzo makini kimedai kuwa, vurugu hizo hazikutokea kwa bahati mbaya bali zilipangwa na wafuasi wa Kiba ambapo inasemekana ziliandaliwa gari aina ya Toyota-Costa zipatazo 25 zilizokuwa zimejaa watu na kwenda kuwamwaga viwanjani hapo kwa shughuli mbili muhimu; kuzomea na kuhamasisha wengine wazomee pindi Diamond atakapopanda jukwaani.
“Ishu ilipangwa, Team Kiba waliibuka na Costa kama 25 hivi, wakajipanga katika maeneo tofauti ya uwanja huo lakini zaidi walikaa karibu na jukwaa ili kuweza kutimiza vizuri azma yao ya kuharibu pindi Diamond atakapokuwa akitumbuiza,” kilidai chanzo hicho.
WALIFANIKIWA?
Kwa namna moja mashabiki hao walionekana kufanikiwa kwani waliweza kuwashawishi watu wengi wazomee kiasi cha kumfanya Diamond ashtukie  na kuamua kutamka hadharani: “Jamani kuna uhuni unaendelea hapa.”
TEAM DIAMOND WACHARUKA
Madai yanasema mara baada ya Team Kiba kufanya vurugu hizo na kufanikiwa, baadhi ya mashabiki ambao waliaminika ni wa Diamond (Team Diamond), walicharuka na kusema hawakubaliani na uhuni huo ambao umefanywa hivyo watahakikisha wanapambana kulipiza kisasi kwa namna yoyote ile.
“Hatukubali, wao si walijipanga hapa kumharibia Diamond, sasa na sisi tutahakikisha tunalipiza kisasi kwa namna yoyote,” walisikika wakisema mashabiki wa Diamond.
BABU TALE AKIRI KUSIKIA
Globalpublshers iliwatafuta Diamond na Kiba ili kujua wanazungumziaje vurugu hizo. Baada ya kumtafuta Diamond bila mafanikio, alipatikana meneja wake, Hamis Taletale ‘Bab Tale’ ambaye alikiri kuwepo kwa maandalizi ya zomeazomea ambayo yalikuwa na lengo ya kumharibia msanii wake.
“Hizi kwetu tumezichukulia kama changamoto, tulisikia kwamba kuna watu wamelipwa kwa ajili ya kufanya fujo lakini hatukujali sana kwani lengo letu si kugombana na mtu, sisi tunafanya muziki mzuri ambao ndoto zetu ni kuufikisha katika levo za Kimataifa,” alisema Bab Tale.
KIBA ANAHUSIKA?
Alipotafutwa Kiba kuzungumzia suala hilo alikataa kuhusika nalo na kudai halina ukweli wowote kwani si rahisi kuwalipa pesa mashabiki wengi kiasi kile waliojitokeza uwanjani.
“Hiyo si kweli ni uzushi tu, sasa mimi nitawalipa nini hao mashabiki wote waweze kumzomea huyo Diamond? Siyo rahisi. Kwanza mimi nifanye hivyo ili iweje? Mimi si mtu wa kushindana na Diamond hata siku moja, nafanya muziki wangu, mashabiki wanauelewa, nashukuru Mungu kwa hilo,” alisema Kiba.

source: Globalpublishers

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment