Friday, October 17, 2014

Bond Adaiwa Kumpa Mimba Mhudumu Wa Bar, Amkana Na Kumtaka Aitoe Mimba.


Bond
Msanii wa filamu Tanzania ambaye ni mtangazaji wa Channel Ten, Bond Bin Sinan, anadaiwa kumpa mimba mhudumu wa bar maarufu ya Break Point (BP) iliyopo Kijitonyama, Dar, anayejulikana kwa jina moja la Grace (pichani).

Grace anayedaiwa kupewa mimba na Bond bin Sinan. 
Akizungumza na Globalpublishers kwa huzuni kubwa, Grace alisema yeye na Bond ambaye kwa sasa anadaiwa ni bwana wa mwigizaji Wastara Juma, walikutana maeneo ya Masaki, Dar, Februari, mwaka huu ambako alikuwa akifanyia kazi awali na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi.
Alisimulia kuwa, katika kipindi hicho walikuwa kwenye mahaba niue ambapo mara nyingi alikuwa akitoka kazini anamfuata nyumbani kwake Mwananyamala, Dar. Aliendelea kufunguka kwamba alipomwambia tu kuwa ana ujauzito wake ndipo mambo yalibadilika huku jamaa akitibuka utadhani kamwagiwa pilipili iliyosagwa.
“Ukweli mwazoni mapenzi yalikuwa shatashata lakini baada ya ujauzito, jamaa aliniruka futi mia.

“Mwanzoni alitaka nikatoe lakini nikakataa na kumwambia kwa nini niue kiumbe kisicho na hatia ndipo  akaingia mitini mpaka leo na ujauzito una miezi sita.
“Kila nikimwambia anasema siyo wake, ananitukana na mwisho aliniambia kwamba nisubiri mtoto azaliwe ndiyo tukapime DNA (vinasaba), sasa nateseka kuulea ujauzito peke yangu.“Naendelea kulea hii mimba, najua Mungu atanisaidia, nitajifungua salama na mwanangu nitamlea lakini inaniuma sana kutokana na majibu anayonipa na matusi ya kila wakati.
Bond Bin Sinan akiwa na Wastara.
“Nimefikia hatua hii ya kuzungumza ili walau mnisaidie jamani maana naona ananisumbua na hanielewi.“Kuna siku nilikutana na aliyekuwa mpenzi wake (Anti Lulu), nikamwambia kila kitu akaahidi kunisaidia,” alisema Grace akimwaga chozi.

 Bond alipotafutwa alisema “Huyo dada mimi simfahamu na ninaona wamepanga kunichafua yeye na Anti Lulu kwa sababu nina meseji nyingi sana za huyo dada, nimewasiliana naye Facebook akisema yupo naye hapo kazini kwake hivyo naomba mpotezee hizo habari siyo za kweli.”
GPL ilifanikiwa kuziona meseji za Bond alizokuwa akiwasiliana na Grace katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambazo zilikuwa zimejaa matusi yasiyoandikika huku akimtaka mwanadada huyo kusubiri ajifungue ndipo wakapime DNA ili kujua ukweli.

Bond alisema hamjui huyo msichana halafu tena sms zake zilizonaswa WhatsApp zikionyesha akisema kuwa asubiri ajifungue wakapime DNA,  DNA ya nini tena wakati ameshasema hamjui huyo dada !

wewe una maoni gani...?

No comments:

Post a Comment