Saturday, September 13, 2014

Steve Nyerere Ajiuzulu Uongozi Kundi La Bongo Movie Unity.

Steve Nyerere
Mwenyekiti wa Club ya Bongo Movie Steve Nyerere amejiuzulu baada ya kuandamwa na kashfa kadhaa ikiwemo ya kudaiwa kufanya kisomo cha wasanii waliotangulia mbele za haki kwa maslahi binafsi.

 Kupitia Instagram Steve aliandika kujiuzulu kwake katika Club hiyo ambayo ni sehemu ndogo tu ya wasanii wote wa filamu nchini ambao wapo chini ya Shirikisho la Filamu Tanzania TAFF linaloongozwa na rais wake wa sasa Simon Mwakifwamba.

"Napenda kuwashukuru ndugu zangu wote, wasanii wenzangu kaka zangu mama zangu rafiki zangu na mimi pamoja na family ayngu nimemua kujiuzulu uongozi wa Bongo Movie nabaki kuwa mwanachama wa kawaida na imani tulifurahi pamoja tukauhuzunika pamoja na daima tutakuwa pamoja"

No comments:

Post a Comment