Monday, September 1, 2014

Rehema Nkalami Kuanzisha Tuzo Za Wasanii Wa Ulaya Wanaotumia Kiswahili Katika Kazi Zao.

Rehema akiwa hewani na muigizaji maarufu wa Tanzania Lucy Komba
Rehema Nkalami mtangazaji maarufu wa Swahili Talk Radio Ya nchini Denmark ambayo hutangaza vipindi vyake kwa lugha ya kiswahili amepanga kuanzisha tuzo kwa ajili ya kuwapongeza wasanii wa sanaa hususani ya filamu na hata muziki katika nchi za Scandinavia ikiwemo Denmark ambapo nchi hizo zipo karibu na wasanii wake hususani wa kiafrika hufanya akzi kwa ukaribu huku wakitoa kipaumbele katika lugha ya kiswahili katika kazi zao.
Rehema ambaye ni mzaliwa wa Tanga, Tanzania amesema kuwa lengo litakuwa kutambua mchango wa wasanii hao katika kukuza sanaa ya kiafrika ughaibuni na kuitangaza Afrika.

Kupitia Swahili Talk Radio Rehema amekuwa akifanya mahojiano na kuwapromote wasanii mbalimbali ambapo wengine pia huwa wenye majina makubwa tayari kutoa Afrika ikiwemo Tanzania.

Sisi tuafikiri ni lengo zuri sana llikifanyiwa kazi. kila la kheri.............

Rehema akiwa na Mr. nice
Rehema akiwa na Abou Twaleb muigizaji wa filamu mtanzania anayeishi Denamark
Rehema akiwa na Safari Lukeka toka VAD Productions
Rehema akiwa na Selembe Toko
Watoto pia hupewa nafasi radioni..............

No comments:

Post a Comment