Wednesday, September 24, 2014

Najuta Kuolewa Mapema, Kumenigharimu Sana Kisanaa Na Kielimu: Nora

 Mwigizaji mkongwe nchini Tanzania Nora Nuru Nassoro amefunguka kuwa siku zote katika maisha yake anajuta kuolewa mapema kwani asingefanya hivyo angeweza kufanya mambo mengi na angekuwa mbali sana kisanii na kielimu.
Akizungumza na Globalpublishers Nora alisema kuwa kipindi alipoolewa na aliyekuwa mganga wa tiba za asili, marehemu Ngwizikulu Jilala, alikuwa akimnyima uhuru wa kuendelea na sanaa na masomo.
“Unajua kweli najuta sana mimi kuolewa mapema kama si hivyo ningeendeleza fani yangu na sasa ningekuwa mbali lakini kipindi chote cha ndoa nilisimama sikuweza tena kuigiza,” alisema Nora.
Msanii huyo amesema kwa sasa amerudi upya kwenye gemu na tayari ameandaa sinema mpya inayokwenda kwa jina la Msimamo Wangu ambayo imeshakamilika, itatoka hivi karibuni.

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment