Thursday, September 25, 2014

Afande Sele Alishutumu Gazeti La Amani Kumuandika Kwa Habari Ya Uongo !

Afande Sele
Gazeti la Amani la leo alhamisi toka Globalpublishers lilikuwa na habari iliyosema kuwa mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini Afande Sele amepata demu mpya siku moja baada ya 40 ya aliyekuwa mkewe kufariki yaani Mama Tunda.
Hata hivyo baada ya kuona habari hiyo Afande Sele ameonekana kuchukizwa na madai hayo kwa kusema ni uongo kilichoandikwa na mwandishi wa gazeti hilo. Kupitia Facebook afande Sele ameandika.........

Wakati flani katika maisha sisi wanasanaa na waandishi wa habari tunahitilifiana kwa kutokuheshimiana tu; na kwa hakika kama tungetanguliza heshima miongoni mwetu daima tusingekwaruzana hata kidogo ukizingatia kuwa tasnia zetu zinategemeana sana,hebu angalia muandishi kama huyu anatumia picha yangu mimi na dada asiemjua halafu bila kuniuliza mimi kama muhusika kuwa huyo dada ninani na anauhusiano gani namimi yeye muandishi moja kwa moja anapeleka picha kwenye mitandao/magazeti na bila aibu,woga na kuheshimu tasnia yake anaandika kuwa'siku moja baada ya 40 ya mkewe afande anamwanamke mpya' wakati si kweli,

NIMEFAIDHAIKA SANA!, ukiachilia mbali suala la kunidhalilisha katika jamii au kunitia ubaya mbele za watu kwa kunisingizia kuwa nimekutwa na mwanamke siku moja baada ya arobaini ya mzazi mwenzangu bado pia sijui hasa huyu muandishi dhamira yake kuu ya kutumia picha hiyo ya kawaida na kuitungia habari ya uongo kama hiyo ilikuwa nini?au ndio tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu?chondechonde ndugu wanahabari kalam zenu mkizitumia vibaya huwa ni silaha nzito kuliko ndege za kivita za jesh la marekani,kwa imani ya dini yangu hata kabla ya kifo cha mzazi mwenzangu ningeweza kuruhusiwa kufunga ndoa na bint mwingine hasa ukizingatia mimi na mama wa hasa ukizingatia kuwa mimi na mama watoto wangu tulikuwa tumeshatengana mwaka mmoja kabla hajafikwa na umauti, lakini kwangu mimi bado sikuwa na sina wazo hilo la kuoa,

No comments:

Post a Comment