Friday, August 22, 2014

Aunty Ezekiel Amjibu Diamond Kuhusu Wema Kupenda Starehe Na Marafiki Wapenda Anasa.

Aunt, Wema na Diamond
Baada ya team Wema kumshambulia Diamond mitandaoni kuwa anamtumia Wema kimaslahi badala ya kumfanya awe na maendeleo na Diamond kuwajibu kuwa Wema haambiliki sababu ya kupenda starehe kupitiliza na marafiki wapenda anasa.
Kauli hiyo ya marafiki wa Wema wapenda anasa ilidaiwa kumgusa moja kwa moja Aunty Ezekiel ambaye ni star wa filamu mara nyingi hata kabla ya kuwa na Wema akidaiwa ni mtu wa kula bata muda mwingi kiasi cha ndoa yake kuonekana ipo ipo tu.

Sasa Aunty alipoulizwa na Bongo5 kuhusu alichokisema Diamond alijibu kwa kusema........

"Diamond alivyoongea pale hakunitaja ina, kwahiyo nikisema kwamba aliongea kwa sababu yangu nitakuwa muongo, yeye aliongea kwa niaba ya watu ambao wako na Wema, hata kama angekuwa amenitja jina sidhani kama angeongea kwamba yule mtu anamfundishwa. Wema ni mtu mzima anaishi mwenyewe na ana maisha yake sidhani kama ni mtu wa kufudishwa, wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu hawajui kuna wakati wa kazi na wakati wa ku-spend maisha"

 Aunty ambaye filamu yake mpya ya Mwajuma Nipe itaingia sokoni hivi karibuni aliongeza kwa kusema "kwa hiyo mimi na muda wangu wa kaz na nina muda wangu wa ku-spend. Sihitaji kunagalia kuna mtu anafuatilia maisha yangu kwamba eti nakuwaga na Wema haiwasaidii chochote. Ninachotakiwa kuangalia nafanya kazi zangu na maisha yangu yanaenda mbele na sitaangalia watu wanasema nini. Mimi nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama anahitajika kubadilika kwasababu Diamond ndiyo anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua mapungufu ya Diamond"


xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu ya MUME BORA tayari ipo madukani nunua nakala yako halisi sasa
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment