Wednesday, July 16, 2014

Wanaigeria Wamtaka Diamond Nchini Germany, Ashley Toto Aitwa Kuweka Mambo Sawa.

Diamond
Superstar wa Bongo Fleva Diamond Platnumz anatarajiwa kufanya show mbili nchini Ujerumani mwezi wa nane mwaka huu. Kwa mujibu wa habari ilizopata SWP ni kuwa show hiyo inaandaliwa na promota wa Nigeria kupitia kampuni ya Britts Events.
Tarehe 29 mwezi wa 8 Diamond atafanya show Essen na tarehe 30 atafanya show Sttutgart. Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa muigizaji wa filamu za kiswahili nchi za Scandinavia Ashley Toto ambaye anaishi Ujerumani ameombwa na waandaaji hao kuwasaidia katika show hizo kutokana na uzoefu wake kwenye mambo ya kuandaa shows za wasanii wa Afrika Mashariki.

                                                                Ashley Toto
                                                      Ashley na Diamond
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment