Tuesday, July 8, 2014

Sio Siri Tena ! Diana Kimaro Na Manaiki Sanga Katika Dimbwi Zito La Kimapenzi.

Diana Kimaro
Sio siri tena ! Mastaa wa filamu nchini Diana Kimaro na Manaiki Sanga ni wapenzi. Juzi SWP ilipenyezewa habari kuwa Manaiki anatoka na Diana Kimaro na kwasasa wameshibana vya kutosha kila mtu yupo hoi kwa mwenzake kama mlenda !.

  Uzuri ni kuwa wakati Swahiliworldplanet ikipewa hot gossip hiyo Manaiki mwenyewe alikuwepo eneo hilo hilo ambapo wasanii kadhaa walikuwa wakifuturu pamoja hivyo SWP haraka sana ikampiga swali la moto Manaiki kama ni kweli yeye na Diana kwasasa ni honey, sweet na mpenzi? Manaiki alibaki kuangua kicheko ambacho kilitoa jibu la moja kwa moja kuwa hajiwezi kwa Diana ambaye kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo anavyozidi kujiimarisha kwenye tasnia ya filamu Swahiliwood.

Pia kupitia mitandao ya kijamii Manaiki amekuwa akiandika ujumbe na kupost picha akiwa na Diana. moja wa ujumbe huo ni huu "#love #never #die japokua haupo na Mimi ila everyday mi naku feel baby sijuwi kupendwa kama we ulivyokua unanipenda na hiyo ni habari ya mjini" 

                                                                  Manaiki

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment