Monday, July 14, 2014

Nipo Single Sikuwahi Kurudiana Na Mke Wangu Halima Ali: Bob Junior

Juzi zilianza kusambaa upya habari kuwa Bob Junior amempa tena talaka mkewe Halima Ali ambaye ni muigizaji wa filamu baada ya kudaiwa kurudiana miezi kadhaa baada ya siku za nyuma kumpa talaka, siku za mwanzo inadaiwa muigizaji Ashley Toto anayeishi Ujerumani alikuwa akitoka kimapenzi na Bob Junior ndiyo sababu ya ndoa kuvunjika, na juzi ikadaiwa ndugu wa Bob Junior wanamuona Halima hana nyota angavu ikidaiwa Bob Junior anashuka kimuziki.

SWP ilimuuliza Bob Junior juzi kama ni kweli ameachana na Halima tena akajaibu "Sikuwahi kurudiana na mke wangu nipo single tokea wakati huo"

Hata hivyo miezi michache zilisambaa picvha zikimuonyesha Bob Junior na Halima wakiwa wamefunga ndoa upya na SWP ilimuuliza Bob Junior na alikubali kuwa waliruidana kweli ila kwasasa jibu lake limezua utata.

Bob Junior na mkewe Halima Ali na mtoto wao
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment