Thursday, July 17, 2014

Lulu Atia Team Kwa Kina Terrence J Kuisaka Namba Ya Simu Ya Justin Bieber !

Lulu
Vile vituko vya reja reja kutoka kwa Tanzanian star actress Elizabeth Michael "Lulu" bado vinaendelea ! habari mpya zinasema kuwa juzi Lulu alienda kwenye seminar ya kuzungumza na wasanii wa Tanzania namna ya kukuza sanaa ya nchini huku watoa mada wakubwa wakiwa mastaa wa Marekani Terrence J, David Banner na Shaka Zulu,.
Kwa mujibu wa habari lengo kubwa la Lulu kuhudhuria seminar hiyo ilikuwa kupata namba za Justine Bieber ambaye amekuwa akiukosha moyo wake kwa miaka takribani 3 sasa. Katika seminar hiyo inadaiwa baada yua jina la Bieber kutajwa Lulu alishtuka na kuushikilia moyo wake kuonyesha ni ni jinsi gani amemuingia moyoni kama si rohoni huku Bieber mwenyewe akiwa hata hamjui Lulu.

Hata hivyo Lulu alipoulizwa na gazeti moja alidai kuwa hakumaanisha moja kwa moja kutaka namba za Bieber licha ya kumzimiakia na siku za nyuma kudai yupo tayari kwa lolote akikutana na Bieber ! vituko vya mastaa hivyo...

                                                            Justin Bieber
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment