Wednesday, July 16, 2014

Dr.Cheni Amwagia Ujiko Sabby Angel.

Muigizaji wa filamu maarufu na mkongwe nchini Muhsin Awadhi 'Dr.Cheni" amemwagia sifa actress Sabby Angel kuwa anafanya kazi kwa bidii sana na atafika mbali kama akiendelea hivyo hivyo. Kupitia Instagram Dr.Cheni aliandika " Sabby Angel msanii anayejituma one day utakuwa msanii mkubwa sanaaaa kwa kuwa unaonyesha uwezo mkubwa"

 Sabby kwasasa anakuja juu kama moto wa kifuu baada ya kucheza filamu ya Hard Price akiwa na Ray, Jackline Wolper na Gabo. amecheza filamu nyingine na Dr.Cheni ambayo bado kuingia sokoni. Filamu zake nyingine alizocheza hivi karibuni ni Moto Wa Radi akiwa na Mohamed Musa, Siri Ya Giningi akiwa na Gabo, na nyingine alizoshuti mwezi ulopita ni Sura Sio Roho akiwa na King Majuto na Tino na ya kwake mwenyewe inayoitwa Sio Riziki ambayo imekamilika editing juzi, Sabby ametengeneza filamu hiyo baada ya Steps kumpa mkataba kama actress/producer. katika Sio Riziki yupo na Tino, Dude, King Majuto na Leo wa Kenya.

unaweza pia kum-follow Sabby kwenye instagram na twitter tayari amejiunga huko............
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment