Thursday, June 26, 2014

Steve Nyerere Akana Uzinduzi Wa Filamu Ya I Love Mwanza Kujihusisha Na Siasa.

 Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie Unity, Steve Nyerere (katikati) akitoa taarifa ya kukanusha uzinduzi wa filamu ya "I Love Mwanza" kujihusisha na masuala ya kisiasa. Kushoto kwa Nyerere ni Sabrina Rupia (Cathy) na kulia kwake ni Wastara Juma na Salama "Sandra" Salmini.
  Katibu wa TAFF mkoa wa Mwanza, Hussein Kimu akiteta jambo na Wastara Juma mara baada ya mkutano huo.
Wastara Juma akihojiwa na Timzoo Karugira wa Azam TV. Picha na Cathbert Angelo wa Kajunason Blog.
--

Baadhi ya wasanii wa tasnia ya filamu Tanzania wanaounda kundi la Bongo Movie  Unity wameomba kutohusishwa na masuala ya kisiasa katika shughuli zao.

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steve Nyerere kutokana na hisia za kuhusishwa kwao katika mambo ya kisiasa mara baada ya kushiriki katika uzinduzi wa filamu ya “I love Mwanza” ambayo ilizinduliwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Waziri wa Utalii, Lazaro Nyalandu.

Steve alisema kuwa wao kama wakuu wa tasnia ya Filamu nchini, hawana mamlaka ya kumtenga mtu katika shughuli zao zaidi ya kumshirikisha mtu yoyote awe mkulima, mfanyabiashara, mwanasiasi bila kujali wa chama gani.

“Membe na Nyalandu wameshiriki katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, wewe subiri uzinduzi mwingine kama utapata nafasi ya kualikwa, lengo letu kubwa ni kuenea sanaa ambayo imezoeleka zaidi mkoani Dar es Salaam, ni mafanikio kwetu,” alisema Steve.

Alisema kuwa kitendo cha kuinadi filamu hiyo mbele ya halaiki ya watu kwenye siku ya uzinduzi wake kilikuwa ni cha kawaida tu kwa sababu hata katika katika nyumba za ibada mambo haya hufanyika, tulifanya wazi bila kificho kwa sababu halikua jambo la haramu ukizingatia ni jambo lililokuwa lina lengo la kusaidia maendeleo ya sanaa nchini katika kukuza kipato cha wasanii wa nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Wasanii wa Filam Mkoa wa Mwanza, Anitha Rwezaura alisema kuwa Membe hakuwa na shughuli nyingine tofauti na zaidi ya uzinduzi wa filamu.

“Ukweli ni huu katika uzinduzi wa filamu ya I love Mwanza ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Bernad Membe ndiyo alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo,  Membe ametokea kuisapoti Bongo Movie siyo dhambi hivyo viongozi wengine wajitokeze kusapoti wasanii kama jinsi alivyo Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, alisema Anitha.

“Tumesikitishwa sana na kusingiziwa mambo ya uongo ambayo hayana ukweli ndani yake na kuhusishwa na masuala ya kisiasa,” alifafanua.

source: Josephatlukaza


Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment