|
Lulu |
Habari mpya ni kuhusu mshiriki wa Big Brother Africa 2013 Nando kuzimika kwenye penzi la star wa filamu Swahiliwood Elizabeth Michael " lulu". akizungumza na
Globalpublishers Nando amesema kuwa anampenda sana Lulu na yupo tayari kumuoa kwasababu ni wife material ingawa bado hajamwambia mwenyewe hilo. Nando pia alisema kuwa anapenda sana kazi za filamu za Lulu na angependa kufanya nae filamu ziku za usoni
"Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake"
Lulu alipoulizwa na mtandao huo alionekana kushtuka na kusema hana na la kusema kama Nando kasema hivyo ""Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema" alisema Lulu ambaye habari zinasema kuwa katika uzinduzi wa filamu yake ya Foolish Age mwishoni mwa mwaka jana alimpa Nando complementary za kutosha ili awe huru na washikaji zake ukumbini.
Nando
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.
No comments:
Post a Comment