Saturday, June 28, 2014

Kutokujua Kiingereza Kunanikosesha Deals Nyingi Katika Kazi Zangu Za Filamu: Richie

Richie
Single Mtambalike "Richie" muigizaji maarufu wa filamu nchini ambaye alianza kuwika kwenye michezo ya kwenye Tv mwishoni mwa miaka ya 1990 kabla ya kugeukia filamu amekiri kuwa lugha ya kiingereza inampiga chenga kiasi cha kukosa deals kadhaa zinazotokana na kazi zake za filamu kutokana na hali hiyo. Akizungumza na Baabkubwa magazine star huyo wa filamu ya Kitendawili iliyotoka hivi karibuni na kupendwa na watu wengi kutokana na kugusia maisha halisi ya kitanzania alisema


 "Kiukweli serikali haipo sambamba na sisi wasanii wa Tanzania tuliokosa kufahamu lugha za wenzetu kwasasa ni shida tupu, mfano mimi lugha ya kiingereza inani-late down coz nashindwa kusonga mbele kufanya movies na stars wengine international but kwa Tanzania ni bonge la star ila nikichukuliwa na nchi jirani u-star wangu unapotea kabisa kisa sijui kubonga kiingereza vizuri, ila najitahidi kuvunja broken English, not only to me wasanii wengi ni tatizo, pia wasanii wa Bongo hawajui nini maana ya filamu na tamthilia coz hakuna filamu yenye part 1 na part 2, wasanii wa Bongo copy and paste inazidi ndio maana tunakuwa na uhaba wa good script writers"

Our Adivece
Kama kweli Richie una nia ya kufika mbali katika kazi zako za filamu basi kutokujua kiingereza kwako sio tatizo na bado hujachelewa kama unayo nia ya dhati ya kujifunza vizuri lugha hiyo. Kwakuwa tayari unazungumza hiyo broken English ni hatua nzuri kuijua lugha hiyo vizuri ukiongeza bidii kujifunza wakati wa muda wako wa ziada na kujisomea magazeti na articles za kiingereza mitandaoni hata kupitia simu yako ambayo unayo mkononi muda mwingi.

Pia jingine la muhimu acha kufanya kazi kwa mazoea ukiwa tayari kama mmoja wa wasanii wakubwa nchini na wanaolipwa vizuri kidogo, ajiri meneja msomi mwenye upeo wa kazi za filamu ndani na nje ya nchi atasaidia sana kufanikisha malengo yako katika mawasiliano na mambo ya mikataba ambayo kwasasa wewe ni rahisi kudhulumiwa bila kujua kama imeandikwa kwa English. Hiki ndicho alichokifanya Diamond Platnumz pia wakati akiwa hajui lugha hiyo huku akijifunza kwa bidii kupitia  Kuigiza kwa english au lugha yoyote ile hata kama huijui sio tatizo kwasababu wapo wasanii wengi wameigiza kwa lugha wasizozijua na kazi zao kupongezwa, kinachotakiwa ni maandalizi ya character na research.

                                                                   Richie

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment