Wednesday, May 28, 2014

ZENA NA BETINA Kuingia Sokoni Tarehe 12 June Na Sio 29 May.

Nisha
"Habari mashabiki zangu,nyumbani kwetu akifa baba au dada au mwanafamilia yyte,basi km kuna aliyetaka kuolewa harusi inaghairishwa,maisha yangu ni filamu,na filamu ni nyumba yangu ya pili,sisi km NISHA'S FILM PRODUCTION NA STEPS INTERTAINMENT tumeamua kughairisha kuitoa filamu yetu mlokuwa mkiisubiri kwa hamu "ZENA NA BETINA" ilikuwa itoke tar.29/05/2014 sasa basi tutaisogeza mbele hadi tar.12/06/14 kwa ajili ya kuomboleza misiba hii,samahani kwa usumbufu uliojitokeza,munisamehe sana,tumeguswa sana,kwangu mm km Nisha kutoa filamu ni furaha,siwezi kufurahi siku tunayomzika msanii mwenzetu kipenzi RACHEL yaani kesho ambayo ndio ilikuwa siku ya kutoka ZENA NA BETINA ,nina imani kubwa kama ingekuwa mimi  filamu isingetoka kesho na hii ni zawadi yenu Rachel na Adam kuambiana kutoka NISHA'S FILM PRODUCTION. .. naomba mnisamehe sana mashabiki wangu, ila nimetazama UTU KWANZA halafu pesa baadae. wanaoendelea kufanya promo wafanye na naomba mnisaidie kusambaza ujumbe huu. . Nawapenda sana. ZENA NA BETINA itatoka tar.12/06/2014 Inshaallah siyo tar.29 tena. Cc @nishasfilmproduction" ameandika Nisha kupitia mtandao mmoja wa kijamii

No comments:

Post a Comment