Saturday, May 17, 2014

William Mtitu Ajenga Nyumba Ya Milion 178.

Filamu zinalipa ! producer na muigizaji wa filamu wa siku nyingi nchini William Mtitu amejenga nyumba mpya ya kisasa maeneo ya Kigogo jijini Dar es salaam. Nyumba hiyo ambayo bado haijakamilika mpaka sasa tayari imegharimu kiasi cha shilingi milioni 178 za Tanzania. Chanzo kimoja makini kikizungumza na GPL kilisema kuwa Mtitu alinunua kiwanja cha nyumba hiyo kwa Milioni 45, milioni 38 kununua samani za ndani na milioni 85 katika ujenzi.

Mtitu mwenyewe ambaye ana filamu nyingi sokoni zinazotamba alipotafutwa kuongelea suala hilo alisema kuwa hana la kusema kwa kuwa kila kitu kinajionyesha.

Mwaka jana Mtitu aliamua kuanza kusambaza filamu zake mwenyewe baada ya muda mrefu filamu zake kusambazwa na msambazaji mmoja ila Mtitu kudai alijitoa katika kampuni hiyo kuepuka unyonyaji wa wasanii uliokithiri ikiwemo kununua haki zote za msanii anapotengeza filamu.

Hii inaweza kuwa moja ya sehemu ya kujifunza kwa baadhi ya wasanii ambao licha ya kuwa tayari na uwezo wa kusambaza kazi zao wenyewe lakini bado wamebweteka na kuishia kulalamika kila siku kuwa wananyonywa. Angalia picha za mjengo wa Mtitu ambao bado kukamilika.......


No comments:

Post a Comment