Friday, May 16, 2014

Ray hawezi Kumuoa Chuchu Hans: Johari

Johari
Muigizaji maarufu na wa kitambo Blandina Chagula "Johari" amesema kuwa habari za Chuchu Hans kuvishwa pete ya uchumba na Vicent Kigosi "Ray" sio za kweli na Ray hatarajii kuoa hivi karibuni na kama tukio hilo ni la kweli basi yeye angejua. Akizungumza na GPL star huyo alisema "Mmh…unasema Ray kamvisha pete Chuchu...! Hakuna jambo kama hilo wewe, achana na matapeli maana hakuna ishu kama hiyo na Ray hawezi kuoa kwa muda huu.”
“Kwani suala la kumvisha pete na kutoa mahari lilifanyikia wapi maana kama kweli kuna mazingira hayo basi atakuwa kafanya kwa kificho sana"

Miezi chache nyuma Johari na Chuchu walidaiwa kurushina ngumi za kufa mtu kwenye ofisi za RJ kisa kikidaiwa ni kugombea penzi la Ray ambaye yeye na Johari ni wamiliki wa RJ Company inayozalisha filamu nchini.
Ray na Chuchu Hans

No comments:

Post a Comment