Saturday, May 10, 2014

Irene Uwoya Na Baba Haji Wadaiwa Kuwa Wapenzi Huku Mahaba Yakiwaelemea.

Uwoya
Irene Uwoya ambaye ni mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu nchini anadaiwa kuwa katika penzi la siri kubwa na muigizaji mwenzake maarufu Haji Adam "Baba Haji". Chanzo kimoja ambacho ni msanii chipukizi wa filamu kilisema kuwa wawili hao ni wapenzi ila imekuwa vigumu hata media kujua kwasababu mara nyingi hujifanya ukaribu wao ni wa kikazi tu kama wasanii wengine huku wakidaiwa kuwa pamoja hasa nyakati za usiku. "Baba Haji na Irene Uwoya ni wapenzi, wanafanya siri sana mi mwenyewe nimeshuhudia Uwoya akimpiga mabusu ya kimahaba Baba Haji na kumuita honey, wananunuliana mpaka zawadi, yaani mahaba yamewaelemea kabisa sema wanashindwa tu kuweka kweupe ili dunia ijue" Chanzo hicho kiliambia Swahiliworldplanet Juzi alhamisi.
Hata hivyo Uwoya na Baba Haji walitafutwa ili kutolea ufafanuzi madai hayo lakini hawakuweza kupatikana mpaka habari hii inaandikwa huku ikidaiwa Baba Haji yupo busy Zanzibar akishuti filamu mpya. Mastaa hao wamecheza filamu kadhaa pamoja kama vile Apple na Last Card

                                                        Haji Adam 'Baba Haji"
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and 

No comments:

Post a Comment