Friday, May 9, 2014

Endless Fame Productions Yatoa Kauli Kuhusiana Na Ugomvi Wa Wema Sepetu Na Kajala

Wema na Martin Kadinda
Kampuni ya Endless Fame Productions inayomilikiwa na Wema Sepetu imetoa kauli yake kupitia meneja wa kampuni hiyo Martin Kadinda kuhusiana na ugomvi wa Wema na Kajala ambao kwa wiki za hivi karibuni wamekuwa wakipamba media hususani magazeti ya udaku na blogs na mitandao ya kimamii mingine. Kupitia Instagram Kadinda ameandika..........


"Good morning all of ypu....I just woke up like "Hasiralees" kwakuwa hili vuguvugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema Sepetu(my client) na Kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe taarifa kutoka kwetu Endless Fame.

Katika urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha  na mwisho wa siku maisha yaendelee hilo ndiyo lililotokea baina ya hawa wawili. Lakini Katika kipindi hicho cha so-called mapumziko kuna mambo mengi yamejitokeza, yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu, kuna media coverage juu ya hawa wawili na Wema sikumpa nafasi ya kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa zaidi, ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana tatizo na Kajala sema tu kwasasa anahitaji space.....tukawa tumefunga mjadala huo

Endless Fame(Wema Sepetu) haijawahi kutamka lolote kuhusu maswala ya mahusiano ya Kajala na mtu yeyote, Endless Fame haijawahi ku-doubt urafiki wa Kajala na any of her friends because tunaamini yale ni maisha yake binafsi na hayahusiani na kampuni ya Wema au Wema mwenyewe, kusaidiana katika matatizo haimaanishi tunammiliki...hapana hapana....hili linaloendelea sasa sisi pia tumelisikia na kuliona kwenye social networks kama watu wengine wanavyoona.

Tunaumizwa na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wana ushahidi kutoka Endless Fame au mtu wa karibu na Wema. Team Wema wote waliopo Instagram sijawahi kuonana na hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza au hatuwezi kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati kwa Wema.

Poleni kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi zetu na maisha yetu maana haya ya Instagram tuyaache huku huku ukiyapatiliza utashindwa kumwamini hata mama yako mzazi"

Hivi karibuni Kajala kupitia kipindi cha TakeOne cha Clouds Tv alisema kuwa ugomvi wao Wema umekuzwa na watu na media na sio kama inavyodaiwa kuwa amemchukulia Wema mwanaume. Kajala alisema kuwa walitofautiana kwa mambo madogo tu ya kawaida lakini wamejikuta wakiwa na ugomvi kweli kutokana na media na watu kuukuza ugomvi huo, Kajala alisema kuwa anaumizwa sana na hali hiyo.
Wema na Kajala
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and 

No comments:

Post a Comment