Wednesday, April 9, 2014

Wema Sepetu Na Mrisho Ngasa Katika Penzi Zito Kwa Siri Kubwa.

Wema Sepetu
Mchezaji mpira maarufu nchini Tanzania Mrisho Ngasa anadaiwa kuwa katika penzi zito na Wema Sepetu ingawa sio kwa muda mrefu sana huku wawili hao wote wakifanya siri kubwa isijulikane. Inadaiwa mrisho amepata nafasi hiyo ya kufaidi kwa Wema baada ya kuanza kuwa karibu na Diamond ambaye ndiye anajulikana kuwa ni mpenzi wa Wema. Habari zaidi zinadai kuwa Mrisho hataki kabisa mambo hayo yajulikane kwenye media kwani hajazoea mikikimikiki ya kuanika maisha yake ya kimapenzi kwenye media wakati Wema akiwa ameshazoea tangu zamani.
Kikizungumza na Habarimpya chanzo kimoja kilicho karibu na wawili hao kilisema "Ngassa na Wema wana mahusiano mazito ingawa mahusiano yao si ya muda mrefu sana lakini katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiyanogesha huku kila mmoja akiyafanya kuwa siri, ingawa kazi kubwa iko kwa Ngassa kwa sababu mwenzake amezoea mikiki ya kuanika mahusiano yake lakini jamaa anaogopa na hapendi kabisa kitu kama hicho kijulikane"

                                                            Mrisho Ngasa
 

 Miezi kadhaa nyuma Mrisho Ngasa pia aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na Snura Mushi ambaye ni rafiki wa karibu wa Wema Sepetu ingawa Mrisho alikanusha madai hayo.



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment