Monday, April 21, 2014

Wema Sepetu Ashinda Taji La Ijumaa Sexiest Girl 2014 Baada Ya Kuwabwaga Lulu, Wolper, Jokate Na Nelly Kamwelu.

Wema akiwa ameshikilia tuzo yake ya Ijumaa sexiest girl 2014
Wema Sepetu ameibuka mshindi wa Ijumaa Sexiest Girl 2014 shindano ambalo lilichukua miezi kadhaa kwa washiriki kupigiwa kura kupitia gazeti la Ijumaa. Katika final waliingia Jackline Wolper, Elizabeth Michael "Lulu", Jokate Mwegelo na Nelly Kamwelu na Wema ambaye jana alitangazwa kuwa mshindi. Hata hivyo baadhi ya watu mitandaoni wameonekana kupinga ushindi wa Wema kwa madai hana lolote zaidi ya kuhamasisha wasichana na wanawake wapuuze ngozi zao za asili na kutumia mkorogo kama yeye ambapo Wema mwenyewe amesema ameshaacha kutumia mkorogo, kwa upande mwingine mashabiki walikubaliana na ushindi wake.

Jackline Wolper ndiye aliyekuwa akilishikilia taji hilo kabla ya kuchukuliwa na Wema huku washindi wengine wa taji hilo miaka ya hivi karibuni wakiwa Irene Uwoya na Wastara Juma.

Congratz Wema

 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment