Friday, April 4, 2014

Risala Ya Kundi La Bongo Movie Unity Ilipikwa: Dude

Dude
Star wa filamu Swahiliwood Kulwa Kikumba"Dude" amesema kuwa risala iliyosomwa juzi katika sherehe za kuadhimisha miaka 3 ya kundi la Bongo Movie Unity imepikwa kwani haikuegemea katika ukweli kuhusu waanzilishi wa Kundi hilo. Akizungumza na Globalpublishers Dude ambaye ametamba na filamu nyingi sokoni na pia igizo la Bongo Dar es salaam alisema "Ile risala imepotosha, Bongo Muvi ilianzishwa na wasanii wa muziki na filamu wakiwemo mimi,  William  Mtitu, H.Baba, Simon Mwakifwamba, MwanaFA na Fid Q na wengineo kwa lengo maalum, nimeshangaa kusikia vile"
Maelezo ya Dude yanashabihiana na alichokisema Simon Mwakifwamba ambaye ni msanii pia na Rais wa Shirikisho La Filamu Tanzania kuhusu waanzilishi wa kundi hilo huku Mwakifwamba akisema kuwa Bongo movie sio chama bali ni kampuni inayomilikiwa na watu tisa na pia sio wanachama wa TAFF na kuongeza kuwa wengine katika kundi hilo wanafuata tu mkumbo wa wasichokijua.




Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment