|
Bond |
Kipindi kinachohusu masuala ya filamu cha Action & Cut kilicho chini ya Bond Bin Sinan ambaye ni mtangazaji, muigizaji, mtayarishaji na muongozaji wa filamu Tanzania kimeingia ubia na Swahili Talk Radio ya nchini Denmark ili kushirikiana na wasanii wanaofanya filamu za kiswahili katika nchi za Scandinavia na ulaya kwa ujumla ambao wanaonekana kupata inspiration kutoka filamu za Tanzania ambazo ndiyo kitovu cha filamu za kiswahili na lugha yenyewe ya kiswahili. Akizungumza na
Swahiliworldplanet Bond alisema "
now kipindi changu cha Action
& Cut kimeingia partnership na kituo cha Swahili Talk Radio cha
Denmark hivyo ni neema kwa wasanii wa Ulaya kufanya interviews moja
kwa moja na zikarushwa katika kipindi changu , pia itakuwa ni neema kwa wasanii wa Scandinavia kujitangaza Afrika
mashariki kwani wengi wao wanafanya filamu za Kiswahili pia jambo lingine ni wasanii wa hapa kuweza kufanya kazi au kushirikiana
na wasanii wa Ulaya kupitia ushirikiano huu. wote kwa pamoja tuna malengo makubwa zaidi ya kuhakikisha filamu za Kiswahili zinafika mbali"
Mtangazaji wa Swahili Talk Radio ya nchini Denmark Rehema Nkalami ambaye anatokea Tanga, Tanzania
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news, life styles news and more
No comments:
Post a Comment