Friday, April 11, 2014

Katu Sitokuja Kutoka Kimapenzi Na Mwanaume Aliyetoka Na Lulu: Diana Kimaro

Lulu na Diana Kimaro katika filamu ya Family Disaster
Star wa filamu Swahiliwood Diana Kimaro amefunguka kuwa kamwe hatokuja kutembea na mwanaume ambaye alishatoka kimapenzi na star mwenzake aliye pia rafiki yake wa karibu Elizabeth Michael "Lulu". Diana alisema kuwa mpenzi wa Lulu ni shemeji yake hivyo hawezi kutembea nae ikifikiriwa kuwa yeye na Lulu ni marafiki walioshibana. " Katu siwezi kufanya hivyo mwanaume yeyote anayemla uroda Lulu mimi ni shemeji yangu hivyo siwezi fanya upuuzi huo" alisema Diana akizungumza na gazeti la Maskani

Diana Kimaro na Lulu tangu waigize pamoja katika filamu ya Family Disaster kama watoto watukutu na baadaye katika Foolish Age walitokea kuwateka mashabiki katika screen.

Lulu na Diana Kimaro katika filamu ya Foolish Age

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment