Thursday, April 10, 2014

Irene Paul Azua Jambo Barabarani.

Irene Paul
Irene Paul ambaye ni star anayetesa katika filamu Swahiliwood jana aliwaacha midomo wazi baadhi ya watu na mashabiki wake maeneo ya Moroco, Kinondoni wakati star huyo alipokuwa ndani ya gari na kutoa chupa ya maji safi na kuanza kunawa mikono barabarani akionyesha alikuwa anapiga msosi ndani ya gari yake yenye rangi ya damu ya mzee wakati akiwa katika foleni za magari ndani ya gari lake.
 Swahiliworldplanet ambayo ilishuhudia tukio hilo la kawaida lakini huwa tofauti linapofanywa na mastaa lilishuhudia baadhi ya watu wakisema kuwa Irene itakuwa kachelewa kupiga msosi sababu ya mishe mishe zake za filamu huku mashabiki wake wakimpongeza kuwa Irene ni mzuri sana akiwa live kuliko kwenye tv. " Irene jamani ananawa barabari, alikuwa anakula itakuwa,huyu dada kumbe ni mzuri hivi ukimuona live" alisema mpita njia mmoja.


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment