Thursday, April 17, 2014

Film Review: Kigodoro Kantangaze - Filamu Yenye Uhalisia Wa Maisha Ya Mtanzania Huku Ikiwa Na Plot Na Picha Duni.

FILM:              Kigodoro Kantangaze
CAST:             Mama Abdul, Diana Kimaro, Kajala Masanja, Riyama Ally, Abdallah Mkumbila, Hemedy Suleiman, Bi.Stara, Salim Ahmed(Gabo)
DIRECTOR:   Jackson Kabirigi
RATING: 3.5/5
Kigodoro Kantangaze ni filamu mpya ambayo kwa asilimia kubwa imebeba uhalisia wa maisha ya mtanzania wa kipato cha chini hasa maeneo ya mjini huku story yake ikiwa imejikita hasa kwa jamii za watu wa mwambao wa Tanzania. Katika hii filamu Mama Abdul ni mke wa Abdallah Mkumbila(Muhogo Mchungu) huku wakiwa na watoto wawili wa kike mmoja akiwa ni Diana Kimaro aliyeigiza kama binti mcharuko huku msichana mwingine akiwa mwenye maadili na mpenda shule. Mama Abdul pia ameigiza kama mwanamke ambaye hajatulia na mwingi wa mambo ya mjini huku akishindwa kutoa malezi malezi mazuri kwa familia yake na matokeo yake binti yake Diana Kimaro kunasa mimba na kupata Ukimwi akiwa bado mdogo. Kwa upande mwingine wanaonyeshwa Kajala Riyama na Bi.Stara nao wakiwa wanawake wenye hekaheka za wasichana wa mjini wa kipato cha chini na kusutana mara kwa mara na kina mama Abdul ambaye pia anaibeba dhima ya madeni pamoja na mume wake katika filamu hiii. Hemedy amecheza kama kijana wa uswahilini mpenda wasichana. Filamu inaisha Diana Kimaro akipata gonjwa la Ukimwi kutokana na tabia zake za mcharuko kwa kukosa malezi mazuri kutoka kwa wazazi wake huku Mama Abdul akiishia kuchukuliwa vyombo vyake vya ndani kutokana na madeni kumzidia.
What is good: Story ya filamu ina visa vinavyoonesha maisha halisi ya mtanzania wa kawaida hasa maeneo mengi ya mjini, kama vile madeni, umasikini, umbea na kusutana, malezi mabaya na mfumo dume kwa wanaume kuendelea kutowapa uhuru wanawake(Gabo na Kajala). Vile vile filamu imefanikiwa kwa upande wa mavazi(costume) kwa wahusika kuvaa mavazi yaliyoendana na sehemu nyingi tofauti na filamu nyingi tunazozishuhudia zikiwa udhaifu upande wa mavazi kwa kuendekeza mavazi mafupi yenye asili ya kimagharibi ambayo hayaendani na matukio halisi. Vile vile location zilikuwa nzuri zikionyesha sehemu na mishe mishe za jiji la Dar es salaam kama story ilivyotaka. Katika hii filamu muongozaji pia alijitahidi kufanya kazi nzuri bila kusahau visa na mikasa toka kwa Mama Abdul, Riyama, Diana Kimaro na Bi.Stara ambavyo vitakufanya ucheke na kufurahi hata kama una stress

What is Bad: Licha ya wazo la story kuwa simple na lenye kuakisi maisha halisi ya mtanzania wa kawaida maeneo ya mjini lakini mwandishi alishindwa kusuka vizuri plot ya filamu hii, visa na matukio yanarukiana sana bila mpangilio maalum kiasi kinachopelekea pia kushindwa kubaini haraka nani ni mhusika mkuu kati ya Mama Abdul na Diana Kimaro ingawa mama Abdul anaonekana kuwa heroine wa filamu hii. Vile vile picha na mwanga wa filamu havikuwa vizuri na kutulia.

Performances: Wasanii wengi walijitahidi kukaa vizuri katika nafasi zao ingawa Kajala na Hemedy walishindwa kuuvaa vizuri uhusika wa uswahilini kiasi cha kuonekana kama mapambo tu katika hii filamu. Kwa ufupi ni kuwa Kajala na Hemedy waliwekwa kwa ajili ya kuuza filamu hii na sio kingine. Abdallah Mkumbila(Muhogo Mchungu) alicheza vizuri katika nafasi yake huku kivutio kikubwa akiwa Mama Abdul mwenye makeke na visa vingi huku akiubeba ipasavyo msemo wa "Kantangaze" ambao kwasasa umekuwa habari ya mjini kwa kinadada na kina mama wengi katika mazungumzo yao si ajabu kuwasikia wakitamka neno "Kantangaze". Mama Abdul alicheza vizuri kiasi cha kutukumbusha enzi za kundi la Mambo Hayo na kutamani kundi hilo lingerudi tena. Kwa ufupi Mama Abdul anastahili nomination ya best actress na hata kushinda kutokana na uhusika wake huo. Kwa upande wa Diana Kimaro nae alicheza vizuri kama binti mcharuko anayechangamkia kila mwanaume na kuishi kupata Ukimwi. Riyama na Bi.Stara pia walicheza vizuri katika nafasi zao licha ya kuwa na limited screen space. Gabo kama kawaida yake alikaa vizuri katika nafasi yake.

Last Word Of The Film: Kama bado hujaiona filamu hii basi hakikisha unainunua na kuitazama maana ni lazima utavunjika mbavu na visa, tambo na makeke ya kina Mama Abdul, Riyama, Bi.Stara, Diana Kimaro huku ukipata funzo pia.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment