Pages

Thursday, March 20, 2014

Yadaiwa Mganga Wa Snura Ndiye Wa Diamond, Snura Ashikwa Na Kigugumizi Cha Kufumwa Kwa Sangoma.

Snura
Jana mitandao mbalimbali ilikuwa na habari kuhusu star wa filamu na muziki nchini Snura Mushi kufumwa kwa mganga wa kienyeji akiwa na tunguli na jogoo huku akifanyiwa ndumba huku picha zake zikinaswa. Baada ya habari hiyo ilibidi Swahiliworldplanet isake ukweli wa habari hizo ikiwemo kumtafuta Snura mwenyewe hata hivyo namba ya Snura hatukuwa nayo so ilibidi kutafuta watu wake wa karibu na kumpata mmoja ambaye ni muigizaji wa filamu pia. Chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina kilisema mapya ikiwemo kusema kuwa Snura kwenda kwa mganga ni mambo ya kawaida kwake na huyo mganga wake ndiye mganga wa Diamond anayewafanya wang'are kwenye sanaa. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo..


SWP: Mzima? naomba namba ya Snura ili kupata ufafanuzi wake kuhusu kufumwa kwa mganga akifanyiwa ndumba.

CHANZO: 071.........(huku akiachia kicheko)

SWP:  Hivi wewe unaonaje ni kweli Snura kaenda kwa mganga ili apae kisanii au ni movie mpya anashuti?

CHANZO:  Mbona mganga anayemtibu Snura ndio mganga wa Diamond(star wa Bongofleva), but kwa hilo la kufumwa sina uhakika nalo yawezekana alikuwa ana-shoot movie

SWP: Hee ! anaitwa nani huyo mganga na anakaa eneo gani?

CHANZO:  Aaah...  mbona kawaida tu we unashangaaaa.

 SWP: Unadhani mafanikio yake kwenye sanaa ni juhudi zake kikazi au huyo mganga?

CHANZO: Ngoja kidogo naongea na mtu kwenye simu....(baada ya dakika kadhaa chanzo kikaendelea kwa kusema), Aahh....kwa muziki gani wa ajabu ?...au kwa viuno gani?

SWP: Basi ahsante kwa ushirikiano wako.

CHANZO: Poaa usinitaje.

SWP: Usijali.

Baada ya kuachana na chanzo hicho mida ya jioni jana SWP ilibidi kumgeukia Snura na kumueleza kila kitu kuhusu issue ya kufumwa kwa mganga akifanyiwa ndumba, Snura alionekana kushtushwa na habari hizo na kukosa jibu la kutoa. Mazungumzo yalikuwa hivi.

SWP: Mambo Snura? hapa ni blog ya Swahiliworldplanet, kuna habari zimesambaa mitandaoni na kukuonyesha kwenye picha kuwa umefumwa kwa sangoma ukiwa unafanyiwa ndumba huku ukiwa na jogoo na tunguli, tungependa kupata ufafanuzi wako kwa ajili ya mashabiki wako.

SNURA: Duh! nyie kiboko (kisha akawa kimya kwa dakika kadhaa)

SWP: Pia inadaiwa kuwa mganga wako ndiye anayempa Diamond nyota ya kupendwa ndiyo maana unakubalika sana kwasasa, je ni kweli ulikuwa kwa mganga au maana picha zinakuonyesha ukiwa na tunguli.

SNURA: Jamanii !

SWP: Ingekuwa vizuri ukafafanua zaidi Snura unajua mashabiki wako wamesoma hizo habari na mitandao kibao imeziandika.

SNURA :(Kimya Snura hakujibu tena mpaka tunaandika habari hizi)

                                                 Snura akiwa mganga


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment