Pages

Thursday, March 20, 2014

Sallai Majasiri Atua Nchini Denmark, Awataka Wasanii Wenzake Wapendane Na Kushirikiana.

Sallai
Sallai Majasiri, Managing director MAJASIRI PRODUCTION ya nchini Uholanzi kwa siku tano sasa yupo nchini Denmark kwa matembezi ya kikazi na kutembelea pia marafiki. Msanii huyo amepokelewa na kundi la V.A.D film production chini ya Safari Lukeka . "Jamani nahisi raha na furaha kwa mapokezi niliyoyapata toka kwa wasanii kwa wasanii na ndugu zangu hawa wa VAD Selembe Toko , Justine zawadi, Claurice Safi ,Rizo babingwa ,Jay msabaha, Papy Gibril ,Richard Muyale , Tatu Tantine, Mungu awabariki zaidi" alisema Msanii huyo anayependa kumtukuza Mungu wakati akizungumza na Swahiliworldplanet


 Sallai ambaye ana mke na watoto aliongeza kwa kusema "Siyo siri nimekuja kwa ajili ya kushiriki katika filamu yao mpya inayoshutiwa kwa sasa na inaitwa MY WIFE , ukizingatia tayari wameshaingiza filamu kadhaa sokoni moja waliyoicheza na Lucy Komba kwa jina la Tanzania to Danmark na nyingine waliomshirikisha mwana Bongo fleva nguli Mr Nice kwa jina la ni Mwamini nani nina furaha kwa hilo, Lakini vile vile nimekuja kutizama namna wenzangu wanavyoandaa na kusimamia kazi zao , nimepata nafasi ya kuongea na uongozi wa VAD kwa maongezi ambayo tutayaweka wazi hivi punde pindi mambo kadhaa wa kadhaa yatakapo kamilika"
 
Sallai akiwa na Lucy Komba

"Nimetembezwa kwingi na kujifunza mengi kutoka kwao ,nimebahatika pia kukutana na dada Lucy Komba ambaye yupo hapa inchini Danmark kwa sasa kwa mapumziko . Wamekuwa mfano mzuri sana kwa makundi yetu hapa Ulaya  maana wanajiamini ndiyo maana hawakuona shaka kunishirikisha katika filamu yao , tofauti na makundi mengi ambayo wanawabania wasanii wengine kushiriki katika filamu zao ,pia kuweka vipingamizi vingi kwa wengine kuwashirikisha au kuchukua wasanii wao . Sote bado tunakua hakuna ambaye alishakuwa star ,bali kuufikia huo u-star itabidi kushirikiana na sio kuzibiana ,na kuringiana maana ujui nani ni nani kesho !" aliongeza zaidi Majasiri ambaye ana asili ya Congo huku akiwa amekaa Tanzania kwa muda mrefu.
 
Sallai akiwa na Selembe Toko
 "Nimeweza kuwasiliana na mmiliki wa Twaleb Entertainment ya mjini Copenhagen ambaye pia aliachia Trailer ya filamu yake ya African Boy kwenye Youtube hivi karibuni, nawasiliana pia na dada Devotha Rose Alfred wa inchini Germany na wengine wengi na kuahidiana kushirikiana kwa ajili ya Swahili European Movies, Kwa hiyo ziara yangu nchini Denmark imekuwa nzuri sana na yenye baraka tele kwa kukutana na watu ambao tulijuana tu kwa mitandao ya kijamii na simu ,lakini sasa tumekua watu wa karibu na kuamua kushirikiana kwa mambo kimaendeleo" Alisisitiza msanii huyo kutambua umuhimu wa wasanii kuungana na kushirikiana.

 Binafsi u-star siyo malengo yangu mimi niko katika filamu kuihubiri injli ya YESU KRISTO kama vile waimbaji wa gospel wanavyo ihubiri kwa njia ya nyimbo , niko hapa kuhubiri maadili mema ,utu amani kwa lugha ya kiswahili kupitia filamu . Mungu wa Mbinguni asifiwe sana , sasa kilichobaki ni kwenda kujiunga na kundi langu la MAJASIRI kwa ajili ya filamu yetu ijayo kwa jina JIPU KANISANI,  Majasiri Production inaongozwa na Gilbert Fataki Pamaoja na Sallai Fataki , huku ikijumuisha waigizaji kama Antoinette kyungu , Jarno Feenstra , Esther Fataki , Kasereka Yowa , Kuba Kone , Espoir Kone , Rosette Sallai , Anniet sijtsma , annepetra Sijtsma , Gladdys Kerubo , Solange Nyarwaka "
 
Sallai

Sallai alimalizia kwa kusema "Nawengine ambao tutawataja baadaye ama mtawaona kwenye filamu zetu hivi karibuni, pia tunashukuru sana kwa wote ambao wanaonyesha moyo wa kutaka kuungana nasi , na wale ambao hawajui ni jinsi gani wanaweza kuwasiliana nasi wanaweza tuma ujumbe hapa kwa nambari hii ya ujumbe sms tu +31 685398905 hiyo ni kwa ajili pia ya mahitaji kuchukua harusi na kumbukumbu za sherehe kadha wa kadhaa wasiliana nasi kwa namba hiyo , Tunaahidi kushirikiana na wote ambao wana nia njema na kwa kufuata utaratibu tuliojiwekea.,Barikiweni mno"

 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment