Odama |
Chanzo hicho kinasema zaidi kuwa mapaparazi hao wamekuwa wakimsumbua Odama kwenye simu kila mara kutaka wampige picha akiwa mjamzito na pia kumuahidi kitita cha pesa akikubali ili picha hizo ziwe exclusive katika gazeti litakalozitoa lakini Odama hataki kabisa kusikia habari ya kupigwa picha akiwa mjamzito na kusambaa kwenye media. "Odama hataki kabisa kupigwa picha na mimba aliyonayo, mapaparazi wengi(akitaja kampuni ya moja ya magazeti) wanamsumbua kila siku na hata kumuahidi kumpa pesa ili wapate picha zake akiwa mjamzito, yaani hataki kabisaa" kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake.
Ukiachilia mbali habari hizo filamu mpya kali kutoka kwa Odama inayoitwa JICHO LANGU inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu. Hakikisha unapata nakala yako halisi.
No comments:
Post a Comment