Pages

Monday, March 3, 2014

Odama Awindwa Usiku Na Mchana Na Mapaparazi Ili Wampiga Picha Na Mimba Aliyonayo.

Odama
Habari mpya zisizo na shaka ni kuwa star mkubwa wa filamu na mwenye heshima kubwa nchini Odama Jennifer Kyaka anawindwa usiku na mchana na mapaparazi ili wampige picha na mimba aliyonayo sasa ambayo ni kubwa kabisa na haijifichi hata kwa asiyeona vizuri. Chanzo makini kimeiambia Swahiliworldplanet kuwa Odama anashinda ndani tu sasa hivi na hata akitoka kwenda sehemu hutoka kwa machale zaidi kwa kuogopa mapaparazi wanaweza kuwa wanamfuatilia na kumpiga picha.


 Chanzo hicho kinasema zaidi kuwa mapaparazi hao wamekuwa wakimsumbua Odama kwenye simu kila mara kutaka wampige picha akiwa mjamzito na pia kumuahidi kitita cha pesa akikubali ili picha hizo ziwe exclusive katika gazeti litakalozitoa lakini Odama hataki kabisa kusikia habari ya kupigwa picha akiwa mjamzito na kusambaa kwenye media. "Odama hataki kabisa kupigwa picha na mimba aliyonayo, mapaparazi wengi(akitaja kampuni ya moja ya magazeti) wanamsumbua kila siku na hata kumuahidi kumpa pesa ili wapate picha zake akiwa mjamzito, yaani hataki kabisaa" kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa jina lake.


Ukiachilia mbali habari hizo filamu mpya kali kutoka kwa Odama inayoitwa JICHO LANGU inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 31 mwezi huu wa tatu. Hakikisha unapata nakala yako halisi.

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment