Lupita |
Ukiachilia mbali suala la Oscar Lupita ameonyesha uwezo mzuri sana kuwa ana kipaji na team yake ni lazima itakuwa makini katika choices za filamu atakazocheza Lupita ili azidi kwenda mbele na sio kurudi nyuma. Lakini baadhi ya watu Hollywood akiwemo mimi tuna wasiwasi kama Lupita kweli atapewa stahili yake katika filamu kama muigizaji mwenye kipaji na sio kupewe nafasi ya filamu kutokana na rangi ya ngozi yake. Hii ni kwasababu mara nyingi waandishi wazungu wa Hollywood hawaandiki roles nzuri na muhimu kwa ajili ya waigizaji wenye asili ya Afrika bali huandika kwa ajli ya wazungu wenzao ambao ndiyo hasa wanaotamba Hollywood kwa kiasi kikubwa, sio kwamba wazungu ndiyo wana vipaji kuliko waigizaji wenye asili ya Africa-America bali ni kutokana na ubaguzi wa rangi kitu ambacho film critics kadhaa Hollywood wamekuwa wakilalamikia.
12 Years A Slave mwandishi na director wake wote ni watu wenye asili ya Afrika na lengo lilikuwa kuonyesha unyama wa wazungu dhidi ya waafrika kipindi cha miaka ya nyuma kitu ambacho wazungu wengi huwa wanakificha. So lupita kupewa characters nyingi muhimu na waandishi wengi wazungu ni kitu ambacho wengi wanafikiria kama itawezekana kutokana na historia ya ubaguzi wa rangi Hollywood kwa waigizaji weusi. Mfano mara nyingi waigizaji wenye vipaji kama vile Gabriele Union kukosa roles wanazopewa waigizaji wa kike wa kizungu licha ya kuwa na sifa.
Wengi wanachoomba ni Lupita kuthaminiwa na kupewa kazi kutokana na kipaji chake siku za mbeleni na sio kutokana na rangi yake. Katika tuzo za Oscar filamu nyingi za waigizaji wenye asili ya waafrika zimekuwa zikipuuzwa kwa miaka mingi.
Kila la Kheri Lupita Nyong'o
No comments:
Post a Comment