Jackson Kabirigi |
Kupitia facebook muigizaji huyo machachari na mmoja wa directors wachache wazuri nchini ameandika hayo hapo chini baada ya hivi karibuni habari kusambaa kuwa Timoth Conrad hataki kuwapa wenzake credit kwenye filamu ambazo wamefanya kazi husika akiwemo Jackson Kabirigi na wiki iliyopita Omary Clayton nae aliibuka na kusema kuwa wameshamaliza tofauti zao na Timothy baada ya kuingia katika mikwaruzano kisa ni credit katika filamu walizofanya kazi pamoja. Kabirigi ameandika.............
"KWA KUFANIKIWA AU KUFA TIMAMU EFFECTS, SIHITAJI BIFU
Kumekuwa na habari kadhaa tokea mimi kukaa pembeni ya kampuni ya Timamu Effects kutokana na
sababu ambazo nimeziona ni za msingi kwangu katika ustawi wa shughuli zangu na kuendelea kuishi
na watu kwa amani.
Pamoja waandishi wa habari hizo kutowahi kunihoji lakini mwenzangu amenitumia ujumbe akidhani
nahusika na habari hizo na naona kuwa nikiendelea kukaa kimya habari hizo zitapelekea kugusana
katika masuala binafsi jambo linaloweza kuleta chuki baina ya tuliokuwa wamiliki wa kampuni
hiyo.
Baada ya hapa sitakuja kuzungumzia tena suala hili....
UKWELI ULIVYO
Tulianzisha Timamu Effects mimi na Timoth Conrad (Tico) kwa kukubaliana kuwa mimi nitakuwa
Producer, Director na Actor wakati mwenzangu atakuwa Editor, Cameraman na ataindesha kampuni
kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufanya mawasiliano. Na tukafanya juhudi kubwa kila mtu afikie
kiwango cha juu kwa eneo aliloshika.
Baada ya mafanikio kuanza kupatikana, mwenzangu akapata wazo kuwa naye awe Producer, Director
na Actor, majukumu ambayo nilikuwa nayafanya mimi katika kampuni. Sikuona ubaya wa mawazo yake
kwa kuwa ni jambo la maendeleo na wala sikuona sababu ya kumbana ila pia sikutaka kusubiri
ifikie wakati tugombanie majukumu, nikaamua kukaa pembeni na kuangalia uwezekano wa kufanya
kazi kwa namna nyingine.
Ieleweke kuwa sina ugomvi binafsi na Tico, tukionana tunaongea kama kawaida na sina kinyongo
naye. Timamu Effects ilikuwa ni biashara yetu na tumetengana kibiashara jambo ambalo ni la
kawaida katika ulimwengu wa biashara. Na sihusiki kwa namna yeyote na Timamu inayotangazwa hivi
sasa.
Kwa sasa najipanga na menejimenti mpya kuona ni kwa namna gani nitatimiza majukumu yangu kwa
amani na kwa ubora zaidi ya ule wa awali. Sina muda wa kujadili mali za kampuni (kama zipo)
kuwa anazo nani na kwa misingi gani, kwa kuwa mali ni vitu vya kupita lakini utu ndiyo kila
kitu kwa binadamu. Ila kwa namna moja au nyingine madeni ya kampuni (kama yapo) siwezi
kuyakimbia, nitayalipa nikitakiwa kufanya hivyo kwa kuwa kwa bahati mbaya hatukuwa na mwongozo
(partneship agreement), tulifanya kazi kienyeji kama ndugu.
USHAURI
Sisi ni vijana na tunatafuta maisha, tujiepushe na mambo yanayopoteza muda katika kufikia
malengo yetu. Namuomba mwenyezi Mungu aniongoze na Inshallah nitafika nitakako."

Timoth Conrod
No comments:
Post a Comment