|
Simon Mwakifwamba |
Muigizaji na muongozaji wa filamu nchini ambaye pia ni Rais wa shirikisho la filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifwamba amekemea baadhi ya watengenezaji wa filamu nchini wanawachukuwa wasichana wazuri barabarani na kuwapa nafasi ya kuigiza kwenye filamu bila kuwa na vipaji na matokeo yake ndiyo huchafua sanaa kwa skendo za mara kwa mara. Akizungumza na Globalpublishers Mwakifwamba alisema "Nakemea wasanii kufanya mambo yasiyofaa mbele ya jamii. Lakini lipo
tatizo moja... unajua mimi nipo kwenye sanaa mwaka wa 28 sasa, nina
uzoefu wa kutosha.
“Siku hizi mambo yamebadilika. Zamani wasanii tulikuwa tunalelewa
kwenye makundi, tulikuwa na wazee wetu ambao walisimamia nidhamu
“Sasa hao ambao wanaokotwa huko barabarani kwa sababu ya uzuri ndiyo
wanaokuja kuharibu sanaa. Watayarishaji wabadilike. Siyo kila miss ni
msanii. Siyo kila msichana mzuri anaweza kuigiza. Wazingatie weledi,
siyo mwonekano."
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news, life styles news and more
No comments:
Post a Comment